Latest News and UpdatesPosted On : 2024-04-17


IFMSO WAKABIDHI MISAADA KWA MLEZI WA KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA CHA AMANI, KILICHOPO ZINGA - BAGAMOYO


Aliyemwakilisha Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha, Dkt Shabani Ngole, akimkabidhi vitu mbalimbali Bi Margareth Mwegala, mlezi wa Kituo cha Watoto yatima cha Amani, kilichopo Zinga – Bagamoyo katika mkoa wa Pwani. Misaada hii ilikusanywa na wanafunzi wa IFM kupitia umoja wao ujulikanao kama IFMSO, na ikaenda kutolewa na viongozi wao pamoja na baadhi ya wanafunzi wenzao. Michango hiyo ilijumuisha vitu kama unga, sabuni, madaftari, viatu, penseli, nk. kwa ajili ya Watoto 36 wanaoishi katika kituo hicho.

Bi Mwegala aliwashukuru wanafunzi kwa kuendelea kusaidia kituo hicho, alisisitiza kuwa kituo bado kina mahitaji mbalimbali ikiwemo kuongeza vyoo kwa ajili ya Watoto hao, na kuweka ukuta Madhubuti kuzuia wezi ambao wamekuwa wakiwasumbua.

PAYMENT PORTAL

BROCHURES

COLLABORATIONS

HEET PROJECT

IFM PROSPECTUS

SHORT COURSES

ALMANAC 2023/2024

CONTACT US

Main Campus
contact our main campus via
P.O Box 3918, 5 Shaaban Robert Street
11101 Dar es salaam
+255 22 2112931-4
Fax : +255 22 2112935
rector@ifm.ac.tz