News Posts

Wanafunzi wa Idara ya Bima wapewa mafunzo na Benki ya CRDB

Zaidi ya wanafunzi 200 wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha wameipongeza na kuishukuru Benki ya CRDB kwa kuwawezesha kupata mafunzo na ujuzi wa namna ya kujiendeleza na kufanikisha taaluma yao katika sekta ya bima.

 

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Mratibu wa Semina, ndugu Eliud Kahige, alisema kuwa hatua ya CRDB kuandaa mafunzo hayo ni ya kupongezwa. Mafunzo yamekuja wakati mwafaka kwa wanafunzi hao ambao wanajiandaa kuingia kwenye soko la ajira. Aliongeza kuwa "Kwa jitihada hizi, nitumie nafasi hii kuishukuru CRDB kwa kutupatia elimu ambayo inatupa maarifa ya msingi kuhusu majukumu yetu ya kitaaluma na namna bora ya kuwahudumia wateja katika sekta ya bima".

 

Kwa upande wake, Meneja Uenezi wa CRDB, alisema kuwa lengo kuu la semina hiyo ni kuwawezesha wanafunzi wa vyuo vikuu, hususan wahitimu, kupata mtazamo mpana kuhusu sekta ya bima, kujenga mitandao, kujitambua kitaaluma na pia kupata msukumo wa kujiendeleza zaidi katika taaluma hiyo. "Ninawasisitiza wanafunzi kuwa licha ya kuwa na vyeti na sifa za kitaaluma, wanapaswa kuwa wabunifu na kuja na bidhaa mpya za bima zitakazokidhi mahitaji ya wateja na mabadiliko ya soko," aliongeza Meneja huyo.

 

Naye, Mkuu wa Kitengo cha Bima wa CRDB Wakala, Bi. Linda Kamuzora, alieleza namna elimu ya bima inavyoweza kuwasaidia wateja, hususani wafanyabiashara wadogo wanaoanza kujitegemea. Alifafanua kuwa kwa kutumia mafunzo hayo, wanafunzi wataweza kuelewa aina mbalimbali za bima zinazoweza kulinda biashara katika mazingira tofauti. "Kumuelewa mteja na kumshauri juu ya aina sahihi ya bima ni jambo muhimu sana, hasa kwa wafanyabiashara wanaochipukia. Bima inaweza kuwa ngao ya mafanikio yao," alisema Bi. Linda Kamuzora.

 

Mkuu wa Idara ya Bima, Bw. Clifford Cosma, aliwashukuru Benki ya CRDB kwa kuwawezesha kitaaluma wanafunzi, na kuwaonyesha fursa mbalimbali zilizopo kwenye kupata na kutumia elimu ya bima. “Mafunzo hay ani muhimu sana kwenu ninyi, na kwa jamii ya Kitanzania kwa ujumla, hivyo myape umuhimu unaostahili,“ alisisitiza.

 

Semina hiyo ni sehemu ya juhudi za CRDB kushirikiana na taasisi za elimu ya juu katika kuwajengea wanafunzi uwezo wa kitaaluma na kuwapa ujuzi wa moja kwa moja unaoendana na mahitaji ya soko la ajira, hususan katika sekta ya bima.


2025-08-04 14:16:33

CAMPUSES AND TEACHING CENTRES

All Campuses of The Institute of Finance Management

STRATEGIC PARTNERS

We are proud working with the best team of strategic partners.

Application Window for September Intake 2025-2026 is Now Open - Click Here to apply

UCHAGUZI 2025
Kujiandikisha kuwa mpiga kura ni msingi
wa uchaguzi bora