News Posts

MAFUNZO YA UTAWALA BORA NA UADILIFU KWA WAJUMBE WA KAMATI MBALIMBALI
“Ni muhimu sana kuwa makini kwenye uadilifu, maana huu ni msingi mkuu wa utumishi wa umma”. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha, Prof Josephat Lotto (Picha ya Chini; katikati – mstari wa waliokaa), Tarehe 24 Mei 2024, alipokuwa akifungua mafunzo ya Utawala Bora na Uadilifu kwa Wajumbe wa Kamati Maalumu ya Menejimenti. Aliongezea kuwa, “uadilifu ndiyo nguzo muhimu katika kuimarisha uwazi na uwajibikaji”. Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku tatu, tarehe 22 – 24 Mei 2024, katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha. Mafunzo ya Utawala Bora na Uadilifu yalitolewa kwa Maafisa Mrejesho na Wajumbe wa Kamati ya Uadilifu (Picha ya Juu), na kwa Wajumbe wa Kamati Maalumu ya Menejimenti (Picha ya Chini). Mafunzo hayo yalitolewa na wawezeshaji kutoka Ofisi ya Raisi – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, na kutoka Ofisi ya Raisi – Ikulu. Lengo lilikuwa ni kuongeza uelewa kuhusu utawala bora kwa wajumbe wa kamati hizo.

2024-05-22 15:56:31

CAMPUSES AND TEACHING CENTRES

All Campuses of The Institute of Finance Management

STRATEGIC PARTNERS

We are proud working with the best team of strategic partners.

Application Window for Postgraduate September Intake 2025-2026 is Now Open - Click Here to apply