News Posts

IFMSO WAKABIDHI MISAADA KWA MLEZI WA KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA CHA AMANI, KILICHOPO ZINGA - BAGAMOYO
Aliyemwakilisha Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha, Dkt Shabani Ngole, akimkabidhi vitu mbalimbali Bi Margareth Mwegala, mlezi wa Kituo cha Watoto yatima cha Amani, kilichopo Zinga – Bagamoyo katika mkoa wa Pwani. Misaada hii ilikusanywa na wanafunzi wa IFM kupitia umoja wao ujulikanao kama IFMSO, na ikaenda kutolewa na viongozi wao pamoja na baadhi ya wanafunzi wenzao. Michango hiyo ilijumuisha vitu kama unga, sabuni, madaftari, viatu, penseli, nk. kwa ajili ya Watoto 36 wanaoishi katika kituo hicho. Bi Mwegala aliwashukuru wanafunzi kwa kuendelea kusaidia kituo hicho, alisisitiza kuwa kituo bado kina mahitaji mbalimbali ikiwemo kuongeza vyoo kwa ajili ya Watoto hao, na kuweka ukuta Madhubuti kuzuia wezi ambao wamekuwa wakiwasumbua.

2024-05-18 00:06:50

CAMPUSES AND TEACHING CENTRES

All Campuses of The Institute of Finance Management

STRATEGIC PARTNERS

We are proud working with the best team of strategic partners.

Application Window for September Intake 2025-2026 is Now Open - Click Here to apply

UCHAGUZI 2025
Kujiandikisha kuwa mpiga kura ni msingi
wa uchaguzi bora