News Posts

TAASISI ZA UMMA ZAPEWA MBINU ZA KISASA NA CHUO CHA IFM

Mafunzo ya "Sustainability Financial Reporting" kwa taasisi za Wizara ya Elimu, Wizara ya Afya, ETDCO, Bodi ya Nafaka Tanzania, Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo  na Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro yanaendelea ambapo leo ni siku ya pili. 

"Sustainability Financial Reporting" ni moja ya takwa la miongozo mipya iliyotolewa na "International Sustainability Standard Board (ISSB)" ya 2021 na kuridhiwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kupitia NBAA Technical Pronouncement and Implementation No. 1 ya 2024 kuhususu Adoption and Implementation of Sustainability Reporting Standards in Tanzania  ya Julai 1, 2024 (rasmi kuanzia Januari 1 2025).

Wawezeshaji wa mafunzo hayo ni CPA Dr Deogratius Mahangila, mkufunzi na mshauri elekezi wa kodi, uhasibu na fedha pamoja na  CPA Yohana Lambo Mayenga, mkufunzi wa Uhasibu na Fedha wa Chuo cha IFM. Mafunzo yalifanyika katika ukumbi wa hoteli ya Kingsway, Morogoro.

IFM inahakikisha mafunzo yake yanaendana na mahitaji ya wakati.

Kwa kujiunga na mafunzo ya awamu ya pili, yatakayofanyika Agosti 2025, tafadhali wasiliana na CPA Yohana Lambo Mayenga
0753427189.

Usikose nafasi hii muhimu


2025-05-15 18:58:55

CAMPUSES AND TEACHING CENTRES

All Campuses of The Institute of Finance Management

STRATEGIC PARTNERS

We are proud working with the best team of strategic partners.

Application Window for Postgraduate September Intake 2025-2026 is Now Open - Click Here to apply