Latest News and Updates



Posted On : 2024-02-02


IFM Alumni wakabidhi vifaa vya TEHAMA


Umoja wa Wanafunzi waliosoma Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM Alumni) wamekabidhi vifaa vya TEHAMA, ikiwemo Projector tatu, kwa uongozi wa chuo hicho mnamo tarehe 19 Disemba 2023.

Zoezi hilo limeongozwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi ambaye pia ni Mwenyekiti wa umoja huo. Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Dkt. Yonazi amesema, wamefikia hatua hiyo mara baada ya kuona umuhimu wa kuongeza vitendea kazi kwa uongozi wa chuo hicho ili kuongeza tija katika masuala ya taaluma.

Naye Mkuu wa Chuo cha IFM Prof. Josephat Lotto amemshukuru kwa namna walivyojitoa na kuona umuhimu wa kufanya hivyo. Prof Lotto ameelezea kuwa hatua hiyo imewapa furaha na faraja, na kupongeza kwa namna walivyojitolea huku akiahidi kutunza na kuvitumia vifaa hivyo kama ilivyokusudiwa.

PAYMENT PORTAL

BROCHURES

COLLABORATIONS

HEET PROJECT

IFM PROSPECTUS

SHORT COURSES

ALMANAC 2023/2024





CONTACT US

Main Campus
contact our main campus via
P.O Box 3918, 5 Shaaban Robert Street
11101 Dar es salaam
+255 22 2112931-4
Fax : +255 22 2112935
rector@ifm.ac.tz