Latest News and Updates



Posted On : 2024-05-27


MAFUNZO YA UTAWALA BORA NA UADILIFU KWA WAJUMBE WA KAMATI MBALIMBALI


Ni muhimu sana kuwa makini kwenye uadilifu, maana huu ni msingi mkuu wa utumishi wa umma”. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha, Prof Josephat Lotto (Picha ya Chini; katikati – mstari wa waliokaa), Tarehe 24 Mei 2024, alipokuwa akifungua mafunzo ya Utawala Bora na Uadilifu kwa Wajumbe wa Kamati Maalumu ya Menejimenti. Aliongezea kuwa, “uadilifu ndiyo nguzo muhimu katika kuimarisha uwazi na uwajibikaji”.

Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku tatu, tarehe 22 – 24 Mei 2024, katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha. Mafunzo ya Utawala Bora na Uadilifu yalitolewa kwa Maafisa Mrejesho na Wajumbe wa Kamati ya Uadilifu (Picha ya Juu), na kwa Wajumbe wa Kamati Maalumu ya Menejimenti (Picha ya Chini). Mafunzo hayo yalitolewa na wawezeshaji kutoka Ofisi ya Raisi – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, na kutoka Ofisi ya Raisi – Ikulu. Lengo lilikuwa ni kuongeza uelewa kuhusu utawala bora kwa wajumbe wa kamati hizo.

PAYMENT PORTAL

BROCHURES

COLLABORATIONS

HEET PROJECT

IFM PROSPECTUS

SHORT COURSES

ALMANAC 2023/2024





CONTACT US

Main Campus
contact our main campus via
P.O Box 3918, 5 Shaaban Robert Street
11101 Dar es salaam
+255 22 2112931-4
Fax : +255 22 2112935
rector@ifm.ac.tz