News Posts

HAFLA YA KUKABIDHI VIKOMBE KWA WANAFUNZI WANAMICHEZO WALIOSHIORIKI MASHINDANO YA SHIMIVUTA 2025

Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha, kwa mara nyingine wamefanya vizuri katika mashindano ya SHIMIVUTA. Na kutokana na ushindi huo, ilifanyika hafla ya kuwakabidhi zawadi mbalimbali. Hafla hiyo ilifanyika hizi karibuni huku Mgeni Rasmi akiwa ni Makamu Mkuu wa Chuo – Utawala, Prof. Jeremia Makindara.

Timu zilizokabidhiwa zawadi ni:
1. 1.Timu ya Mpira wa Kikapu (Wanawake) – Mabingwa
2. Timu ya Mpira wa Kikapu (Wanaume) – Mabingwa

Zaidi ya hayo, wanamichezo bora pia walipongezwa. Wanamichezo hao (na kategoria zao) ni:
1. Maria Mbena – Mchezaji Bora (MVP)
2. Fares Daniel Kunubwi – Mchezaji Bora (MVP)
3. Emmanuel Samir – Mlinzi Bora (Best Defender)
4. Esther Thomas – Mkimbiaji Bora wa Magunia
5. Moro Berly Tatu – Mwanariadha Bora wa Mbio za Mita 400
6. Veronica Maro – Mwanariadha Bora, na,
7. Shomari Kabulola – Kocha Bora.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mgeni Rasmi aliwapongeza wanamichezo, makocha na viongozi wa michezo. Juhudi walizozifanya zimekiwezesha Chuo kupata mafanikio makubwa katika mashindano ya SHIMIVUTA 2025.

Aidha, alisisitiza umuhimu wa wanafunzi kuwa na ujuzi wa ziada, hususani katika michezo, kwani huongeza thamani yao katika soko la ajira katika nyakati hizi za ushindani mkubwa. Alieleza kuwa michezo huwajengea wanafunzi nidhamu, uwezo wa kufanya kazi kwa pamoja, uongozi na kujiamini, sifa ambazo zinahitajika katika ulimwengu wa ajira wa sasa.

Hafla hiyo ilihitimishwa kwa kukabidhi vikombe na kutoa pongezi kwa washindi, pamoja na kupiga picha za kumbukumbu na viongozi wa Chuo.

 


2026-06-02 13:15:28

CAMPUSES AND TEACHING CENTRES

All Campuses of The Institute of Finance Management

STRATEGIC PARTNERS

We are proud working with the best team of strategic partners.

Application Window for Certificate, Diploma, Postgraduate Diploma, Masters - September Intake 2026-2027 and PhD is Now Open - Click Here to apply