News Posts

CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA WAKABIDHI MISAADA YA KIBINADAMU KWA AJILI YA WAATHIRIKA WA MAFURIKO YALIYOTOKEA KIBITI NA RUFIJI, APRILI 2024

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kibiti, Bi. Mariam Katemana (aliyesimama kulia), akipokea, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa na Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Mheshimiwa Kanali Joseph Kolombo, baadhi ya misaada ya kibinadamu kutoka kwa Dkt. Eugene Mniwasa (wa pili kutoka kushoto), Mwenyekiti wa Kamati ya Muda Maafa ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), jana tarehe 16/08/2024. Pamoja nao, ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti, Bw. Denis Kitali (wa pili Kushoto), na Bw Juma Kibacha, kutoka IFM (wa kwanza kulia).

 

Wafanyakazi wa IFM, Chama cha Wafanyakazi wa Elimu ya Juu (RAAWU) tawi la IFM, na Chama cha Akiba na Mikopo IFM (IFM SACCOS) walichanga fedha (zaidi ya TShs 6,400,000/), nguo na vifaa mbalimbali kwa ajili ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea katika wilaya za Kibiti na Rufiji mwezi Aprili 2024.


2024-08-17 09:27:13

CAMPUSES AND TEACHING CENTRES

All Campuses of The Institute of Finance Management

STRATEGIC PARTNERS

We are proud working with the best team of strategic partners.